INFINIX XCLUB-INFINIX MOBILITY COMMUNITY OFFICIAL FORUM

 找回密码
 Register
Search
Hot search: XStore
View: 270|Reply: 5

ULINZI NA USALAMA WA WATOTO NI JUKUMU LETU SOTE

[Copy link]

68

Threads

262

Posts

330

Xpoints

content partner

sign star1sign star2post star1

Post time 2020-03-26 19:41:04 From the mobile phone | Show all posts |Read mode
Mtoto ni Nani?[br][br]Mtoto ni mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane (18). Tafsiri hii imetokana na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto, Mkataba wa Afrika kuhusu Haki na Ustawi wa Mtoto, Sera ya Maendeleo ya Mtoto na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya 2009. Katika umri huu mtoto anahitaji malezi bora ili aweze kuishi vizuri, kushirikishwa, kulindwa na kuendelezwa kiakili kwa ajili ya maisha yake ya baadae ya utu uzima. Katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 6:6 “Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena, uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo” kwa kusudi la kuwapatia malezi bora.[br][br][br][br][br][br][br]Haki za Mtoto.[br][br]Watoto wana haki za kipekee kwa sababu ya umri wao mdogo na hali yao ya utegemezi ambayo inaweza kuwafanya wadhulumiwe na kutendewa vitendo vibaya. [br][br]Watoto wote wana haki sawa bila kujali jinsia, rangi, kabila, dini, hadhi au hali ya afya. Umoja wa Mataifa, Serikali, wazazi/walezi na jamii kwa ujumla wana wajibu wa kuhakikisha watoto wanapatiwa haki zao. Yesu hakutaka haki za watoto zidharauliwe, Mathayo 18:10b “Angalieni msidharau mmojawapo wa wadogo hawa” na katika Mathayo 18:3 anasema “Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi”. Yesu alionyesha utetezi wa haki za watoto nasisi tufuate kielelezo chake.[br][br]Haki za mtoto zimegawanyika katika makundi makuu manne (4) yafuatayo:[br][br][br]i. Haki ya Kuishi: Inahusu kulinda na kuendeleza uhai wa mtoto ikiwepo:[br][br]- Kuzuia magonjwa na kupata huduma za matibabu, [br][br]-Chanjo na kufuatilia ukuaji [br][br]-Lishe bora [br][br]- Mavazi yanayositiri[br][br]- Makazi salama[br][br]-Maji saf na salama[br][br]- Usaf wa aina zote[br][br][br]ii. Haki ya Kuendelezwa: [br]Mithali 22: 6 inasema “mlee mtoto katika njia impasayo nae hataiacha hata ataka-pokua mzee”. Maendeleo ya mtoto kiakili yanajumuisha:[br][br]-Elimu (rasmi na isiyo rasmi)[br][br]-Tamaduni, mila na desturi sahihi za jamii yake.[br][br]-Kiroho[br][br]-Vipaji[br][br][br]iii. Haki ya kulindwa: Kuhakikisha mtoto analindwa dhidi ya:-[br][br]-Unyanyasaji na ubaguzi[br][br]-Ukatili (kimwili, kingono na kihisia)[br][br]-Unyonywaji ikiwa ni pamoja na ajira za utotoni[br][br]-Ukeketaji, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia[br][br]-Mazingira hatarishi[br][br]-Kutelekezwa au kuachwa bila mlezi[br][br]Biblia inaonyesha jinsi wazalisha wa kiebrania walivyowalinda watoto na kuwanusuru na kifo dhidi ya amri ya mfalme iliyotolewa kwao nyakati hizo, haya tunayasoma katika [br][br]kitabu cha Kutoka1:15. Akasema, wakati muwazalishapo wanawake wa kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa[br]ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi. Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu wasifanye kama walivyoamriwa na Mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.[br][br]iv. Haki ya kushiriki[br][br]Kundi hili linahakikisha kwamba watoto wanapatiwa nafasi ya kutoa mawazo na kwamba maoni yao yanazingatiwa hasa katika maamuzi yanayo athiri maisha yao. Mtoto anapaswa kushirikishwa katika ngazi zote kuanzia kwenye familia, jamii na taifa. Katika Biblia tunaona jinsi Yesu alivyopendezwa na sifa kutoka vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao, [br]haya tunayasoma katika Mathayo 21:15-16 “Lakini wakuu wa makuhani an waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, [br]Mwana wa Daudi! Walikasirika”. Katika ushiriki huu wa watoto Yesu alitetea na kusimama upande wa watoto wala [br]sio upande wa maoni ya viongozi wa dini.[br][br]Wajibu wa wazazi/jamii katika [br]kuhakikisha watoto wanapatiwa haki [br]zao.[br][br]Watoto ni Baraka, Zab: 127:3 ”Tazama wana ndio urithi wa BWANA, uzao wa tumbo ni thawabu.” Na katika Marko 10:13 Biblia inasema “Basi wakamletea watoto wadogo ili awague” jamii ina wajibu wa kuwapeleka watoto kwa Yesu katika nyanja zote za maisha, kielimu, kiroho, kijamii na kiuchumi. Hivyo basi, wazazi/walezi wana wajibu wa;-[br][br]1. Kuwahudumia watoto wao na kuhakikisha wanapata mahitaji yao ya msingi. [br][br]2. Kuhakikisha kwamba watoto wanalindwa dhidi ya magonjwa, wanapelekwa kwenye chanjo, wanapatiwa huduma za afya na lishe bora. [br][br]3. Kuwaandikisha shule, kufuatilia maendeleo yao shuleni na kuwapatia mahitaji yote ya shule.[br][br]4. Kushirikisha, kuongoza wanashirikishwa, kuongozwa na kuhakikisha watoto wanatimiza wajibu wao kikamilifu ikiwa ni pamoja na kufuata imani, tamaduni sahihi, kuzingatia masomo, kujilinda, kujifunza na kusaidia kazi za nyumbani zisizo athiri elimu, afya na zinazoendana na [br]uwezo wa mtoto.[br][br]5. Kuwalinda watoto dhidi ya kunyanyaswa, unyonywaji, kutelekezwa, kufanyiwa ukatili na kuchukua hatua pale ambapo haki za mtoto zimevunjwa. [br][br]6. Kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kuhakikisha huduma zinapatikana kwa viwango stahiki [br]katika maeneo yao.

This post contains more resources

You have to Login for download or view attachment(s). No Account? Register

x
Reply

Use magic Report

418

Threads

4167

Posts

4585

Xpoints

Content Partner

Rank: 8Rank: 8

singel medal2020 Wish MedalXClub Best Look20Msign star1sign star2sign star3sign star4Xclub Kolsign star1post star1post star2sign star2sign star3

Post time 2020-03-26 20:00:10 From the mobile phone | Show all posts
asante kwa elimu
Reply

Use magic Report

318

Threads

6942

Posts

7314

Xpoints

Security Supervisors

Rank: 8Rank: 8

couple medalACTIVE STAR2020 Wish MedalXClub Best Look20M4.0xclub2019sign star1sign star2sign star3post star1post star2sign star4X'Club badge exclusive for Tanzania

Post time 2020-03-26 20:01:27 From the mobile phone | Show all posts
ahsante sana kwa kutujuza
Reply

Use magic Report

68

Threads

262

Posts

330

Xpoints

content partner

sign star1sign star2post star1

 Author| Post time 2020-03-26 20:02:51 From the mobile phone | Show all posts
Karibu Tena ujifunze mengi zaidi
Reply

Use magic Report

68

Threads

262

Posts

330

Xpoints

content partner

sign star1sign star2post star1

 Author| Post time 2020-03-26 20:03:41 From the mobile phone | Show all posts
by Namtamwa | 2020-03-26 20:01
ahsante sana kwa kutujuza
Your welcome,
Reply

Use magic Report

3651

Threads

210K

Posts

310K

Xpoints

Jade Diamond LV36

POP OUTChocolate Day MedalHug Day MedalKiss Day MedalPromise Day MedalPropose Day Medalsingel medal2020 Wish Medalpost star1post star2post star3Xclub Kolpost star3sign star2post star4post star5sign star3X'Club badge exclusive for India

Post time 2020-03-30 00:56:13 From the mobile phone | Show all posts
good share
Reply

Use magic Report

You have to log in before you can reply Login | Register

Points Rules

Infinix Official Website|Infinix official mall|infinix Note 4|INFINIX XCLUB-INFINIX MOBILITY COMMUNITY OFFICIAL FORUM

GMT+8, 2020-04-10 12:02 , Processed in 0.068034 second(s), 21 queries .

Powered by Discuz! X3.4

© 2001-2017 Comsenz Inc.

快速回复 返回顶部 返回列表